9/4/16

Mimba 51 zabainika madarasani


 
 Wanafunzi 74 wamesimamishwa masomo katika shule mbalimbali za sekondari na msingi Manispaa ya Dodoma, kutokana na kupata mimba, huku Mkuu wa wilaya hiyo, Christina Mndeme akisema wametoa picha mbaya ya ujio wa makao makuu ya nchi.
Kati ya wanafunzi hao; wa sekondari ni 45 na kati yao 23 ni wa kidato cha nne.
Alisema wanafunzi sita ni wa shule za msingi wanaokadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 13 hadi 14, wa sekondari wengi wana umri kati ya miaka 16 na 15.
Akizungumza ofisini kwake jana, Mndeme alisema wanafunzi hao walibainika katika Kampeni ya ‘Niache Nisome Magauni Manne’ ambayo inalenga kumpatia nafasi mtoto wa kike asome hadi kufikia malengo anayoyataka.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm