9/6/16

Mrema Adai Maandamano Yanaongeza WafungwaMwenyekiti Bodi ya Parole ,Augustine Mrema amesema maandamano ni uhaini na chanzo kinachotengeneza wafungwa watarajiwa nchini.

Mrema amesema hayo leo kupitia mkutano wake na Kamishna Mkuu wa Magereza nchini ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.

"Haiwezekani inji(nchi) hii ikiwa ya maandamano tu.Enzi ya rais Kenyatta ilikuwa hata ukifikiria tu kwamba atakufa lini ,tayari unakuwa umefanya kosa kisheria, sasa hautaki au unataka Rais ni Magufuli ,sasa wasisababishe ongezeko la wafungwa watarajiwa ndiyo maana nilizungumza na bodaboda na wale dada poa pale uwanja wa fisi ili kupunguza kasi ya wafungwa watarajiwa,"alisema.

Pia ameagiza Jeshi la Magereza nchini kutoridhika na manufaa ya wafungwa kupitia ya sheria ya Parole na bad ala yake ifanyiwe maboresho ili kusaidia kupungua kwa wafungwa wengi gerezani.

Sheria ya Parole ya 1994 ilifanyiwa maboresho yake mwaka 2002 katika kifungu change 4 na kupungua idadi miaka kutoka minane hadi minne kwa mfunguwa anayetakiwa kunufaika na Parole. 

Chanzo: Mwananchi
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts