9/1/16

Msajili amlima barua Maalim Seif malalamiko la Lipumba


OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa imemwandikia barua Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, ikimtaka kujibu malalamiko ya aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba.


Aidha, ofisi hiyo imeutaka uongozi wa chama hicho kueleza hatua ulizopitia hadi kufikia uamuzi wa kumvua uenyekiti na kumsimamisha uanachama msomi huyo.

Ofisi hiyo imeupa uongozi wa CUF hadi kesho saa 9:30 alasiri kuhakikisha umejibu barua hiyo uliouandikia.

Agosti 29, Prof. Lipumba aliwasilisha malalamiko kwenye ofisi hiyo akipinga kuvuliwa uenyekiti na kusimamishwa uanachama wa CUF.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm