9/17/16

Mtatiro afunguka sakata la utekaji vigogo wa CUF
Mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya CUF, Julius Mtatiro

Mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya CUF, Julius Mtatiro amelitaka jeshi la polisi kuchukua hatua dhidi ya watu wanaohusika na majaribio ya utekaji wa viongozi wa chama hicho kabla wanachama “hawajachukua hatua zao”.

Kauli ya Mtatiro imekuja baada ya Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano wa chama hicho, Mbarala Maharagande kueleza uwepo wa jaribio hilo la utekaji na kukamatwa kwa wahusika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa watuhumiwa watatu wanaendelea kuhojiwa kutokana na jaribio la kumteka Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha wa CUF, Jorah Bashange.

Mtatiro amewaambia wanahabari leo mchana kuwa ni vyema polisi wakaona mfululizo wa vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyofanywa na wafuasi wanaodaiwa kumuunga moja ya vigogo wa zamani wa chama hicho.

Mtatiro amesema wana ushahidi wa kutosha juu ya vijana hao wanaojaribu kuteka viongozi wa chama hicho.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts