9/4/16

Mtatiro: Maalim Seif hana sababu ya kubembeleza

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi CUF, JuliusMwenyekiti wa Kamati ya Uongozi CUF, Julius Mtatiro amesema katibu mkuu wa chama hicho, Maalim Seif hana sababu ya kujibembeleza kwa Rais wa Zanzibar, Dk Mohamed Shein kwa sababu masuala ya maslahi kwa viongozi wastaafu ni ya kikatiba na kisheria na hayatolewi kwa hisani ya mtu.

Akizungumza leo kufuatia kauli ya Rais John Magufuli jana akiwa ziarani visiwani humo kwamba Dk Shein asingesaini posho na matibabu kwa ajili ya Maalim Seif kwa vile alikataa kusalimiana naye, Mtatiro alisema viongozi wastaafu wanastahili kupata matibabu na posho nyingine kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi.

“Tunataka kumweleza Rais Magufuli kwamba Dk Shein hana uwezo wa kufuta matibabu na posho kwa Maalim Seif kwa kuwa yapo kikatiba na kisheria,”alisema.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts