9/25/16

MUGABE:Bara la Afrika lipo tayari kujiondoa Umoja wa Mataifa.


Rais ROBERT MUGABE wa Zimbabwe amesema Bara la Afrika lipo tayari kujiondoa Umoja wa Mataifa  iwapo madai yake ya kutaka kufanyika mabadiliko kwenye umoja  huo hayatatekelezwa.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana leo, Rais MUGABE amesema Umoja wa Afrika  unajiandaa kuunda kundi  la kusimamia kujitoa likijumuisha mataifa mengine kama vile Urusi,  China  na  India  iwapo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa halitajumuisha wanachama kutoka kwenye bara la Afrika mwakani.
 
Kiongozi huyo wa muda mrefu Barani Afrika ametoa kauli hiyo alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa  Kimataifa wa Harare  ambako alipokewa na kuhutubia mamia ya wanachama wa Chama cha ZANU-PF waliokwenda kumlaki.
 
Alikuwa akirejea kutoka New York ambako alipata nafasi ya kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambako alizilaumu nchi za Magharibi kwa kuchochea uchumui wa nchi yake kuwa mbaya zaidi.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm