9/20/16

Mwanafunzi Mbaroni Akituhumiwa Kumuua Mwenzake kwa Mti wenye Msumari


MWANAFUNZI wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Mwali iliyopo Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma mwenye umri wa miaka 14 (jina limehifadhiwa), amekamatwa na polisi akituhumiwa kumuua kwa kumpiga kichwani kwa mti wenye msumari mwanafunzi mwenzake.
Tukio hilo lilitokea Jumatano iliyopita, saa 12:00 jioni katika Kijiji cha Mwali, wilaya ya Kasulu mkoani humu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinard Mtui, alisema chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi kati ya wanafunzi hao.
Kamanda Mtui alisema mwanafunzi huyo alifariki dunia kutokana na kuvuja damu nyingi kichwani baada ya kupigwa kwa mti wenye msumari.
Kwa mujibu wa Kamanda Mtui, mwanafunzi aliyepoteza maisha katika tukio hilo ni Riziki James (14), aliyekuwa akisoma darasa la tano katika shule hiyo.
“Mtuhumiwa tunamshikilia na tunaendelea na upelelezi, ukikamilika tutampeleka mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake,” alisema Kamanda Mtui.

-chanzo: NIPASHE
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts