9/15/16

Mwenge wawaibua walimu Kahama

 
Mbio za mwenge wa uhuru unaotarajiwa kuingia wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga, zimezua jambo, baada ya Chama cha Walimu (CWT) kupinga walimu wasikatwe fedha zao.
Halmashauri ya Mji wa Kahama inadaiwa kupanga kuwakata walimu Sh30,000 kwa mwezi kwa ajili ya kununua vitenge vya sare.
Mwenyekiti wa CWT wilayani humo, Victor Tandise amesema mshahara ni mali ya mtumishi na haupaswi kukatwa bila idhini yake.
Amesema walimu wa halmashauri ya mji huo na Msalala watanunua vitenge hivyo kwa hiari yao na siyo kwa kuwalazimisha.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Deogratias Kapami amesema uamuzi huo waliupitisha ili kuwasaidia walimu wasio na  fedha.
Amesema kila mtumishi wa umma anapaswa kushiriki mkesha wa mbio hizo kitaifa kwa mwaka huu.
“Kama kuna mtumishi amejipenyeza na kuingia nchini wakati sio Mtanzania, basi apinge kushiriki mkesha huo, lakini kama ni Mtanzania lazima ashiriki akiwa amevaa sare,” amesema Kapami.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts