9/5/16

Mwingine Aongezeka afikishwa kortini akidaiwa kumuua dada wa bilionea Msuya

MFANYABIASHARA wa jijini Arusha, Revocatus Evarist (40), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam akikabiliwa na tuhuma za mauaji ya Aneth Msuya, dada yake bilionea wa madini ya Tanzanite, marehemu Erasto Msuya.
Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo mwishoni mwa wiki.
Kufikishwa mahakamani kwa mshtakiwa huyo kunafanya idadi ya washtakiwa wanaodaiwa kumuua Aneth, sasa kufikia wawili.
Awali, mke wa bilionea huyo, Miriam Msuya, naye alifikishwa mahakamani hapo akikabiliwa na shtaka kama hilo.
Evarist alisomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Magreth Bankika.

Nipashe
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts