9/7/16

Picha: Katika kikao cha pili bungeni leo.


Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Harrison Mwakyembe akiwaeleza jambo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (Kushoto) Mhe. Ruth Mollel na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt Abdallah Possi. Wakati wa Kikao cha Pili cha Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Leo Mjini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimueleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (MB) wakati wa kikao cha 2 cha bunge la Jmahuri ya Muungano wa Tanzania
Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamisi Kigwangalla akijibu swali wakati wa Wakati wa Kikao cha Pili cha Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Leo Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Yusuf Masauni akijibu swali wakati wa Wakati wa Kikao cha Pili cha Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Leo Mjini Dodoma. 
Picha na Hassan Silayo

Shindano la “SHINDA GARI NA WHITEDENT” laendelea Mikoani.

Baadhi ya Wananchi wa Mkoa Kigoma wakiangalia moja ya gari kati ya magari 25  yanayoshindaniwa  wakati wa uzinduzi wa  shindano la shinda gari na Whitedent linaloendeshwa na kampuni ya kutengeneza dawa ya meno ya Chemi cotex linaloendelea hivi sasa nchini ili kuadhimisha miaka 25 ya kampuni hiyo.
Baadhi ya Wananchi wa Mkoa wa Kigoma wakiwa katika foleni ya kwenda kujisajili kwenye droo ya bahati nasibu wakati wa uzinduzi wa  shindano la shinda gari na Whitedent linaloendeshwa na kampuni ya kutengeneza dawa ya meno ya  Chemi cotex linaloendelea hivi sasa nchini ili kuadhimisha miaka 25 ya kampuni hiyo.
Baadhi ya Wananchi wa Mkoa wa Singida wakijisajili kwenye droo ya bahati nasibu wakati wa uzinduzi wa  shindano la shinda gari na Whitedent linaloendeshwa na kampuni ya kutengeneza dawa ya meno ya  Chemi cotex linaloendelea hivi sasa nchini ili kuadhimisha miaka 25 ya kampuni hiyo

Taswira mbalimbali Bungeni Mjini Dodoma.


Baadhi ya Wabunge wakiingia katika ukumbi wa bunge kuhudhuria kikao cha 2 cha bunge la kumi na moja  la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mbunge wa Jimbo la Urambo Mhe.Margaret Sitta akimueleza Jambo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo Mjini Dodoma.

Naibu Waziri Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akijibu swali wakati wa kikao cha 2 cha bunge la Jmahuri ya Muungano wa Tanzania ambapo alitoa wito kwa waajiri nchini kuwasilisha nyaraka za wastaafu kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii miezi mitatu hadi sita kabla ya kustaafu kwa wateja wao ili kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (MB) akimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba Leo Bungeni Mjini Dodoma.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kintinku  mkoni Singida wakifuatili vikao vya Bunge leo Mjini Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akijibu swali wakati wa kikao cha 2 cha bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo alisema serikali haina mgogoro wowote wa mafuta baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, wakati wa kikao cha Pili cha Bunge hilo leo Mjini Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (MB) akimueleza jambo Mwansheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju leo Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Andrew Chenge akiongoza kikao cha Bunge leo Mjini Dodoma

Mbunge wa Jimbo la Kaliua Mhe. Magdalena Sakaya akiuliza swali wakati wa Kikao cha Pili cha Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts