9/4/16

Polisi wapiga risasi hewani kutawanya wafuasi wa CUF


Wafuasi wa CUF wakisikiliza maelekezo kutoka

Jeshi la polisi limefyatua risasi kadhaa hewani kuwatawanya wafuasi wa chama cha wananchi CUF wanaodaiwa kuwa ni wapambe wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Prof Ibrahim Lipumba ambao walifika katika ofisi za chama hicho zilizopo Buguruni jijini Dar es Salaam.
Hali hiyo imezua taharuki kwa wafanyabiashara wa soko la Buguruni huku gari la polisi likiwa limeimarisha ulinzi katika ofisi hizo hadi mkutano huo ulipomalizika ambapo wafuasi hao walifika katika ofisi hizo wakati viongozi wa chama hicho wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari na wakizungumza na mwandishi wetu baadhi ya wafuasi hao baada ya kutawanywa wameelezea azma ya wao kwenda katika ofisi hizo.
 
Katika mkutano na waandishi wa habari, mwenyekiti wa kamati ya uongozi wa chama hicho, Julius Mtatiro, akijibu maswali mbalimbali likiwemo la wafuasi hao kufika katika ofisi hizo amesema chama kina taratibu zake na kinaendeshwa kwa mujibu wa katiba na kuhusu ujio wa askari hao katika ofisi hizo amesema.
 
Chama hicho kimeitisha mkutano huo ili kuelezea masuala mbalimbali ya kisiasa yanayoendelea hapa nchini na kuhusu msimamo wa chama chake huko visiwani zanzibar amesema.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts