9/25/16

Rais Magufuli ateua Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI

004
Aliyekuwa Mganga Mfawidhi hospitali ya Rufaa ya Dodoma Dkt. Zainabu Chaula (kushoto) ambaye Rais Magufuli amemteua  kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI ) katika moja ya matukio  hospitali ya rufaa ya Dodoma akionekana kukabidhiwa msaada wa mto wa kulalia na Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kati,Mruta Hamisi kwa ajili ya wodi ya watoto hospitalini hapo.
…………………………………………………………………………..
Rais Magufuli amemteua Dkt. Zainab Abdi Seraphin Chaula kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuanzia leo tarehe 24 Septemba, 2016.
Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Zainab Abdi Seraphin Chaula alikuwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Dkt. Zainab Abdi Seraphin Chaula anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Dkt. Mtasiwa ambaye amestaafu.
Dkt. Zainab Abdi Seraphin Chaula ataapishwa Jumatatu tarehe 26 Septemba, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm