Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

9/13/16

Sakata la CUF, Profesa Lipumba lawaibua wanachuo
Profesa Lipumba
Jumuiya ya vyuo vikuu ya CUF, tawi la Mlimani, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), limedai kuwa aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba anatumiwa na CCM ili kukigawa.
Hata hivyo, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula amewajia juu vijana hao akisema Profesa Lipumba ni msomi mashuhuri hapa nchini na kamwe hawezi kutumiwa kwa masilahi ya chama kingine.”
“Hizo tuhuma siyo za kweli, Lipumba ni profesa, msomi na amekiongoza chama hicho kwa muda mrefu. Hawezi kutumiwa, they are not fair to him (hawajamtendea haki),” alisema Mangula na kuongeza kuwa Profesa Lipumba ana heshima yake.
Profesa Lipumba mwenyewe hakupatikana kuzungumzia madai hayo kwani alipopigiwa simu iliita bila ya kupokewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi (SMS) hakujibu.
Akizungumza na vyombo vya habari jana jijini hapa, mwenyekiti wa tawi hilo, Jidawi Chande alisema Profesa Lipumba amekuwa akipita kwenye vyombo vya habari na kupotosha umma kwamba yeye bado ni mwenyekiti wa CUF jambo ambalo ni kinyume na katiba ya chama hicho.
Alisema vijana wa CUF, tawi la Mlimani wanaunga mkono uamuzi wa Baraza la Uongozi la CUF lililoketi Agosti 28 na kuamua kuwasimamisha uanachama Profesa Lipumba na wenzake kwa sababu chama hicho kinafuata katiba na kanuni zilizowekwa.
“Chama ni taasisi na sio mali ya mtu binafsi. Mtu yeyote hatavumiliwa kama hatafuata misingi ya katiba yetu, awe Mtatiro (Julius, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi) au Maalim Seif (Sharif Hamad, Katibu Mkuu). Tunamtaka Profesa Lipumba aache kukihujumu chama, amekitumikia kwa muda mrefu na tunatambua mchango wake,” alisema Chande.
Mwenyekiti huyo alisisitiza kwamba lazima uamuzi mgumu ufanyike ili kulinda katiba ya chama na kuondoa ubinafsi wa viongozi.
“Profesa Lipumba hana nia ya kuijenga CUF, bali anataka kuivuruga. Anachokifanya ni kukihujumu chama kwa masilahi yake binafsi ... Hatutakubali kugawanyika kwa sababu ya tumegundua dhamira yake,” alisema.
Katibu wa CUF, Tawi la Mlimani, Razaq Malilo alitoa wito kwa wanachama wa chama hicho kujipanga kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019 na Uchaguzi Mkuu wa 2020.

mwananchi