Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

9/8/16

Serikali na mkakati mpya kufufua vyuo vya maendeleo
MSEMO wa Kiswahili ‘elimu ni ufunguo wa maisha’ unatumia maneno machache kuonesha umuhimu mkubwa wa elimu kwa binadamu.

Wazungu pia wana msemo wao kwamba “kama unadhani elimu ni ghali, jaribu ujinga!” Katika kukabaliana na umuhimu wa elimu, tumeshuhudia jitihada mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanywa na jamii katika kuhakikisha watoto wanapata elimu ili kwayo iweze kuwasaidia katika maisha yao ya baadaye. Tumeshuhudia pia wazazi wakiwa tayari kutumia kiasi kikubwa cha pesa kupeleka watoto wao shule na vyuoni, wakilenga kuona wanapata elimu bora ambayo itakuwa jibu la ustawi wao wa baadaye.

Halikadhalika, katika jamii yetu wapo ambao walitamani kupata elimu kwa maana ya elimu rasmi ili iwasaidie katika malengo yao mbalimbali ya maisha, lakini wakashindwa kutimiza ndoto hiyo kwa sababu mbalimbali. Moja ya sababu ambazo zimekuwa zikikwaza upatikanaji wa elimu, hususani kwa familia zenye kipato duni ni uwezo mdogo wa kifamilia katika kuwaendeleza watoto wao. Hali inakuwa ngumu zaidi kama elimu yenyewe inapatikana nje ya kijiji au mkoa wao huku pia ikiwahitaji kuzama kwenye mifuko yao ili kuilipia.

Katika mazingira hayo, tumeshuhudia serikali na wadau mbalimbali wakijitahidi kadri wanavyoweza ili kusaidia watoto wa Watanzania wanapata elimu. Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDC) ni matokeo ya mipango ya serikali katika kuwapa wananchi wake elimu inayozalisha wataalamu wanaohitajika katika jamii kwenye eneo husika kwa ajili ya maendeleo ya jamii husika. Vijana wanaopata elimu katika vyuo hivi humaliza elimu yao wakiwa pia na stadi mbalimbali za ufundi.

Baada ya zaidi ya miaka 40 ambayo vyuo hivyo vimekuwa vikitoa elimu na hapo nyuma kuonekana kama vinalegalega, sasa serikali imeamua kuandaa mpango maalumu wa kuvifufua na kuviendeleza. Lengo ni kukidhi matakwa na vigezo vya kuanzishwa kwake kwani umuhimu wa vyuo hivyo bado uko pale pale na pengine umeongezeka.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Stella Manyanya, akiwa ziarani mkoani Kigoma, anasema kuwa kwa sasa vyuo hivyo ni muhimu sana katika kuwaunganisha wananchi, hasa wa vijijini, katika wakati huu ambao nchi inajipanga kuelekea kwenye uchumi wa viwanda. Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, vyuo vya maendeleo ya wananchi ambavyo hapo awali vilikuwa chini ya wizara hiyo, vinakabiliwa na hali mbaya ya uendeshaji.

Kwa sasa serikali imeamua kuviweka chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi ili kuboresha muundo wake, ikiwa ni pamoja na kuchukua wanafunzi wa kutosha. Taarifa zinaonesha pia kwamba, mbali na tatizo la uendeshaji, vyuo vya maendeleo ya jamii pia vinakabiliwa na uchakavu wa majengo, uhaba wa vifaa vya kufundishia na uhaba wa walimu hasa wenye taaluma za masomo husika.

Katika taarifa yake kwa Naibu Waziri, Mkuu wa chuo cha FDC Kibondo, Robert Kihwele, anasema chuo hicho pia kuna changamoto za uchakavu wa majengo, uchakavu wa miundombinu ya umeme na huduma muhimu za kijamii. Kadhalika, anasema huduma ya chakula imekuwa pia mbaya kutokana na madeni makubwa yanayodaiwa na mzabuni. Taarifa hiyo ya Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibondo haitofautiani na taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Kasulu, Hellena Shemweta.

Yeye pia anasema chuo chake hakitoi mvuto kwa jamii kujiunga nacho. Ni kutokana na hilo, Shemweta anaiomba serikali kupitia kwa Naibu Waziri iangalie mpango wa kuwapangia kwenye vyuo hivyo wanafunzi wanaomaliza darasa la saba ili viweze kupata wanafunzi wa kutosha. Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDCs) vingi vilianzishwa kati ya mwaka 1965 na 1969 na ndipo mwaka 1970 serikali ilipitisha sheria rasmi ya kuanzishwa na kutambuliwa kwa vyuo hivyo.

Taarifa zinaonesha kuwa moja ya madhumuni makubwa ya vyuo hivyo ilikuwa ni daraja la kuwaendeleza wanafunzi na watu wazima ambao hawakupata elimu na hivyo kujiunga na mafunzo ya ufundi yaliyokuwa yakitolewa na vyuo hivyo baada ya kuhitimu elimu ya watu wazima. Pia baadhi ya wanafunzi ambao walimaliza darasa la saba lakini hawakupata nafasi ya kuendelea na masomo maeneo mengine walipata pia nafasi ya kujiunga na vyuo hivyo kwa ajili ya fani ambazo ziliwasaidia kujiunga na Veta au vyuo vingine nchini.

Naibu Waziri Manyanya anasema kuwa madhumuni na nia ya kuanzishwa kwa vyuo hivyo vya maendeleo hayajabadilika na yataendelea kuwa yale yale ingawa yapo maboresho ya kumuundo na uendeshaji yatafanywa kuwawezesha wanafunzi wanaomaliza vyuoni hapo kujiunga na Veta.

“Vyuo hivi bado ni muhimu, serikali imeamua kuviweka chini ya Wizara ya Elimu ili kuboresha na kusimamia kwa karibu uendeshaji wake, shida kubwa vilikuwa havipati ruzuku na ndiyo maana vimechakaa na havina mvuto kwa jamii. “Tutabadilisha yote haya na hasa wakati huu ambapo soko la ajira la uchumi wa viwanda linahitaji vijana kama nguvu kazi wenye taaluma mbalimbali,” anasema Naibu Waziri.

Kauli hii ya Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Stella Manyanya inaweza kuwatia moyo na kurudisha ari ya vyuo hivi ambavyo viko maeneo mbalimbali nchini ambapo vijana watakaojiunga navyo watafaidika na elimu watakayopata na hasa wale ambao watakosa nafasi kwenye vyuo vingine.

“Tunajua shida ambayo vyuo hivi vimepitia, havina nyenzo za kufundishia na matatizo mengine mengi lakini kwetu sisi vyuo hivi vikishirikiana na Veta ni vyuo muhimu katika kuwafanya vijana wetu waweze kujiajiri baada ya kumaliza mafunzo yao,” anasema Manyanya. Anasema katika mwaka huu serikali imetenga fedha itakayotumika kuvifanyia ukarabati mkubwa baadhi ya vyuo hivyo na kwamba ukarabati utakuwa unafanyika kwa awamu.