9/19/16

Serikali yalifunga gereza la kilimo la Kitengule wilayani Karagwe.


Serikali imelifunga kwa kipindi cha majuma mawili gereza la kilimo la Kitengule lililoko katika wilaya ya Karagwe ambalo kuta zake zilianguka kufutia tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera na kufanya uharibifu mkubwa wa nyumba za makazi na majengo ya taasisi za kiserikali pamoja na kusababisha vifo vya watu 17.
Agizo la kufungwa kwa gereza hilo limetolewa na waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba baada ya kutembelea gereza hilo na kujionea madhara yaliyosababishwa na tetemeko, amesema wafungwa 280 waliokuwa wakiifadhiwa kwenye gereza hiyo watahamishiwa kwenye gereza la Mwisa na wafungwa 100 watahamishiwa kwenye makambi madogo ya gereza hilo.
 
Kwa upande wake waziri wa elimu, sayansi na teknologia Profesa Joyce Ndalichako ambaye pia ametembelea shule mbalimbali za sekondari na za msingi zilizoathirika kufuatia tetemeko la ardhi amesema serikali iko kwenye mchakato wa kuzikarabati shule hizo, naye mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Matopeni Grace Mshemba ameonyesha kusikishwa na utaratibu wa unaofanywa na serikali wa kusambaza chakula cha msaada kwa waathirika huku Josephina Josephat muathirika wa tetemeko ambaye ni mlemavu akiilalamikia serikali.
 
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm