9/5/16

Serikali yapiga marufuku watoto kuchunga Ng’ombe mkoani Pwani.


Serikali wilayani Rufiji mkoani Pwani imepiga marufuku tabia ya watoto kuchunga ng'ombe huku ikitoa siku kumi kwa wafugaji kuondoa mifugo yao katika maeneo ambayo hayakupangwa kwa ajili ya mifugo na kurejea katika maeneo yao kama mpango wa matumizi bora ya ardhi unavyoelekeza katika maeneo husika.
Mkuu wa wilaya ya Rufiji mkoani Pwani Bw Juma Njwayo ametoa agizo hilo wakati akijibu kero za wananchi wa  kata ya Muhoro waliokuwa wakilalamikia wafugaji kuachia mifugo kuharibu na kula mazao yao na kuliagiza jeshi la polisi kufanya kazi hiyo baada ya siku hizo.
 
Awali wananchi wa kata ya Muhoro na vitongoji vyake walitoa kero mbalimbali ikiwemo rushwa katika mabaraza ya ardhi kwa kuwapa haki wenye pesa.
 
Katika hatua nyingine wananchi hao wamekubali uwekezaji wa kiwanda cha sukari cha Agro Forest katika maeneo yao baada ya kuridhishwa na hatua ya serikali kusimamia hatua zote za uwekezaji na uchukuaji wa ardhi katika maeneo yao ambayo nao watanufaika na uwekezaji huo.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm