9/26/16

Serikali yatangaza vita na walima bangi, mirungiSerikali imetangaza vita vikali dhidi wa wananchi wanaolima madawa ya kulevya aina ya bangi pamoja na mirungi badala ya mazao ya chakula.

Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemerry Senyamule amesema kifungo cha miaka 30 kitawahusu wananchi wa wilaya yake wanaolima mirungi badala ya mazao ya chakula na biashara kwani mbali na kuleta madhara kwa afya zao wanapozitumia lakini pia kuisababishia Serikali hasara kutokana na kutolipa kodi.

Mkuu huyo aliyasema hayo leo alipokuwa alikabidhiwa mradi wa ujulikanao kama Ruvu Muungano uliojumuisha zahanati sita, nyumba mbili za waganga, matanki saba ya kuvuna maji pamoja na madarasa 54 ofisi 16 za walimu, vyumba na vyoo vya chuo cha ufundi Makanya uliofadhiliwa na shirika la World Vision Tanzania. 
 
chanzo: Mwananchi
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts