9/22/16

Shule zilizoharibiwa na tetemeko zakarabatiwa

SERIKALI kupitia kamati ya maafa ya mkoa kwa kushirikiana na Idara ya Uratibu wa Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, imeanza kuchukua hatua za kurejesha miundombinu ya shule za sekondari za wavulana za Ihungo na Nyakato kwa kuanza kubomoa majengo yaliyoharibiwa na tetemeko la ardhi.Tetemeko hilo limeelezwa kuwa na ukubwa wa 5.9 katika vipimo ya majanga hayo kimataifa, na kwa mujibu wa mtandao wa kompyuta wa earthquaketrack.com ndilo kubwa zaidi katika historia kutokea nchini.

Hatua za kuanza kubomoa majengo ya shule hizo, zimeanza kuchukuliwa baada ya kamati ya maafa kutoa misaada mbalimbali kama huduma za afya kwa majeruhi, huduma za mahema na maturubai na chakula ili waathirika kujihifadhi baada ya kupoteza nyumba zao.

Hata hivyo, Serikali ya Japan ilimuahidi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wiki iliyopita kwamba ingechukua jukumu la ukarabati wa shule zote zilizoharibiwa na tetemeko mkoani Kagera, katika hafla maalumu iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu alikitaka kitengo cha maafa katika Ofisi yake kuwasiliana na Japan kwa ajili ya kuwezesha ushiriki wa nchi hiyo katika ukarabati huo.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm