Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

9/12/16

Tetemeko lingine ltokea tena usiku wa kuamkia leo huko Kagera

Tetemeko lingine la ardhi limetokea tena usiku wa kuamkia leo huko Kagera kwenye Manispaa ya Bukoba ambalo limewafanya baadhi ya wananchi kulala nje kuhofia usalama wao.


Taarifa zilizotoka mkoani humo zimedai kuwa tetemeko hilo halikuwa kubwa tofauti na lile lililotokea siku ya Jumamosi na kusababisha vifo vya watu 16 na wengine 253 kujeruhiwa, nyumba 840 kubomoka na nyingine 1264 zikibakia na nyufa.

Wakati huo huo mabweni ya shule ya sekondari ya Nyakato yakiharibika kabisa na kusababisha wanafunzi wa shule hiyo kukosa mahali kwa kulala.

Awali akiongea baada ya kutembelea waathirika wa tetemeko hilo, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliwataka wakazi ambao nyumba zao zimeharibiwa kutorejea tena wenye nyumba hizo kutokana na kutofahamika kama tetemeko hilo lingerudi kwa mara nyingine.

“Tuna wasiwasi kuwaingiza tena kwenye mabanda yale, tukiwalaza tena hapo halafu kama litarudi tena jioni tunaweza kuwa na hadithi nyingine tena mbaya sana. Mtatuvumilia, tuombe muwatumie wataalamu wetu wa hali ya hewa na wengine wanaofanya kazi ya kuangalia shughuli zilizopo chini ya ardhi, kama huu mtikisiko ni endelevu au umekuja kwa muda mfupi,” amesema Waziri Mkuu. Aidha rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli amehirisha ziara yake ya siku tatu nchini Zambia ikiwemo kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais wa sita wa nchi hiyo, Edgar Lungu kwa ajili ya kufuatilia maafa hayo yaliyotokea mkoani Kagera na kumuagiza Mama Samia Suluhu kumwakilisha kwenye ziara hiyo