9/19/16

Ujenzi wa Reli Mpya ya Kati Kuanza Desemba

 rail
Ujenzi wa reli mpya ya kati ya Standard gauge unatarajia kuanza Desemba mwaka huu, baada ya serikali kukamilisha taratibu za zabuni za kumpata mkandarasi atakayefanya kazi hiyo.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, wakati yeye na baadhi ya wabunge waliposafiri kwa treni kutoka Dodoma hadi Dar es Salaam.

Aidha, Waziri huyo wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, akafafanua juu ya taratibu za kuhakikisha reli ya sasa ya kati, inapitika katika kipindi chote cha mwaka.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la reli (TRL) Bw. Masanja Kadogosa akathibitisha kuwa pamoja na kujengwa kwa reli mpya, reli ya zamani itaendelea kutumika.

Katika safari hiyo ya treni kutoka Dodoma hadi Dar es Salaam, mmoja wa wabunge Bibi. Riziki Shahani Mngwali, ambaye ni mbunge wa viti maalum (CUF) Mafia, akaeleza ameionaje safari hiyo.

Hawali, wasafiri waliokuwa katika stesheni Dodoma, wakielekea mikoa ya Tabora na Kigoma, walipata fursa ya kuonana na waziri na kuelezea changamoto mbalimbali wanazozipata kupitia usafiri huo wa reli, na waziri pamoja na menejimenti ya (TRL) wakawahakikishia kuwa zitatafutiwa ufumbuzi wa kudumu, ili waweze kusafiri bila ya tatizo lolote.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm