9/1/16

Ulimwengu kutoongeza mkataba Mazembe

MSHAMBULIAJI wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Thomas Ulimwengu , amesema kuwa hatasaini mkataba mpya na klabu hiyo baada ya ule wa awali kumalizika.
Hata hivyo Ulimwengu alikataa kuweka wazi muda ambao mkataba wake na klabu hiyo unatarajiwa kumalizika.
Akizungumza na gazeti hili jana, Ulimwengu alisema kuwa sasa hivi 'ameshaiva' na yuko tayari kwenda kucheza soka la ushindani katika klabu za Ulaya.

Ulimwengu alisema kama angekuwa na mkataba mfupi na mabingwa hao wa zamani wa Afrika hapo mwaka jana angeweza kusajiliwa na klabu moja ya Ufaransa, lakini ilishindikana kutokana na muda wa mkataba wake uliobakia.

"Ndoto zangu ni kwenda kucheza Ulaya , na kiwango nilichofikia si cha kwenda kufanya majaribio kama wachezaji wengine wanavyokwenda, mimi nitaenda kusaini moja kwa moja," alisema mshambuliaji huyo.

Aliongeza kuwa anasikitika kuikosa Nigeria lakini anaamini kukaa kwake nje kutamsaidia apone vizuri majeraha na kurejea tena uwanjani akiwa na nguvu mpya.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm