9/8/16

UNESCO lapongeza hatua ya Rais Dkt. John Magufuli kutoa elimu bure nchini.

Image result for unesco
Shirika la elimu, sayansi na utamaduni la umoja wa mataifa  UNESCO limepongeza hatua ya Rais Dkt. John Magufuli kutoa elimu bure na kusema kuwa hiyo ni hatua ambayo inatakiwa kuchukuliwa na nchi zingine za Afrika ili kuhakisha kuwa watoto wa leo wanakuwa na uhakikia wa maisha ya kesho.
Hayo  yamesemwa na mwakilishi mkazi wa shirika hilo hapa nchini  Bi. Zulimira Rodrigues wakati wa maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa siku ya  kisomo dunia ambapo amesema jitihada zinazaofanywa na serikali ya awamu ya tano  katika mambo ya elimu zinazotoa mwanga mzuri  kwa Taifa.
 
Naye kaimu kamishina wa elimu kutoka wizara ya  elimu na mafunzo ya ufundi Bw. Nicolas Bureta  amesema nchi inajitahidi kuhakikisha kuwa inaboresha  kiwango cha elimu nchini na kuhakisha wanafunzi wanapata elimu bure.
 
Kwa upande wake mkurugenzi wa elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi  Bi. Basiliana   Levira amesema licha ya jitihada kubwa zinazofanywa kuhakisha watu wanajua kusoma  na kuandika lakini bado wapo watu ambao hawajui.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts