9/18/16

Upungufu wa Walimu Unakwamisha Kasi ya Elimu Bora

Kila mwaka kuna ongezeko la wanafunzi wanaojiunga shule za sekondari lakini wasiwasi wangu mkubwa ni kuwa, ongezeko hilo limekuwa haliendi sambamba na idadi ya walimu wanaojiunga na taaluma hiyo.

Kila mwaka kuna ongezeko la wanafunzi wanaojiunga shule za sekondari lakini wasiwasi wangu mkubwa ni kuwa, ongezeko hilo limekuwa haliendi sambamba na idadi ya walimu wanaojiunga na taaluma hiyo.

Matokeo ya hali hiyo utakuta shule nyingi zina wanafunzi wa kutosha, lakini zina upungufu mkubwa wa walimu.

Kwa mazingira kama haya, tunajikuta tukipiga hatua moja mbele na kurudi hatua mbili nyuma.

Hata hivyo, jitihada zikiweza kufanywa tutaweza kulimaliza tatizo hili, hasa kwa kuongeza mafunzo na kutoa motisha hasa ili kupunguza wimbi la walimu wanaoamua kuacha kazi hii kutokana na mazingira magumu.

Hata hivyo, tunaishukuru sana serikali kwa hatua hii kwa kuwa wazazi wengi tuliokuwa tunashindwa kuwapeleka watoto wetu kwenye shule za sekondari za binafsi baada ya kukosa zile za serikali sasa tunajua wataweza kwenda kwenye shule hizi.

Ninaona ni jambo la maendeleo kwa kuwa sote tunajua kuwa elimu ndiyo ufunguo wa maendeleo.

Nilikuwa ninashauri kuwa wakati tumeweza kupiga hatua kwa kuwa na shule nyingi basi sasa tuanze kuziboresha bila kuangalia uwezekano wa kufungua nyingine.

Hii itawezekana kwa kuweka nguvu kubwa zaidi katika kuongeza idadi ya walimu na maslahi yake ili walimu wengi waweze kubaki kwenye taaluma hiyo.

Kutokana na uhaba huo wa walimu, baadhi ya shule walimu waliopo wanalazimika kufundisha masomo yote hata kama hawayamudu inavyopasa. Sasa hapa hizo ni kasoro kwenye elimu hiyo.

Vile vile, kuwawezesha wanafunzi kusoma hata masomo ya sayansi zianze kujengwa maabara za sayansi ili wanafunzi waweze kufundishwa masomo hayo ya sayansi.
Rafiki wa elimu,
Singida
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts