9/16/16

Utasa wamsababisha aibe mtoto wa siku 10

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich
Utasa ni hali ya mwanamke ambaye amefikia umri wa kuzaa lakini hawezi kupata mtoto. Hatua hiyo, husababisha msongo wa mawazo kwa mhusika, hali iliyomkuta mkazi wa Kipawa jijini Dar es Saalam, Anna  Luambano  (33).
Anna amelazimika kuiba mtoto kutokana na kuwa tasa.
Mwanamke huyo anashikiliwa na polisi Mkoani Morogoro kwa tuhuma za  kumuiba mtoto mwenye umri wa siku 10 wa Maimuna Mahmoudu (20) ambaye ni mkazi wa  Chamwino, Manispaa ya Morogoro.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema tukio hilo lilitokea  Septemba 13 asubuhi kutoka kwa mama  yake.
Mtei alisema polisi walifanya msako na kumnasa  mtuhumiwa maeneo ya Mdaula akisafiri kwenda  Dar es Salaam.
Alisema mwanamke huyo alimrubuni Maimuna ampe mtoto ili akamuonyeshe shemeji yake kuwa mdogo wake amejifungua na awape fedha wagawane.
Mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa hilo katika Hospitali ya Kata ya Mafisa.
Kamanda Matei alisema mtuhumiwa anahojiwa  na hatua za kumfikisha  mahakamani zinafuata.

CHANZO: Mwananchi
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts