Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

9/6/16

WADAU WAJADILI MPANGO KAZI WA KUENDESHA SHUGHULI ZA SERIKALI KWA UWAZI (OGP) WA AWAMU YA TATUBaadhi ya wadau waliohudhuria mkutano wa kujadili Mpango Kazi wa Kuendesha Shughuli za Serikali kwa Uwazi ( OGP)  wa Awamu ya Tatu  wakimsikiliza  Katibu Mkuu Ikulu  Bw. Peter Ilomo (hayupo pichani) wakati akiwasilisha hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es Salaam. 


Mkurugenzi Mtendaji wa TWAWEZA Bw. Aidan Eyakuze akichangia mada katika mkutano wa wadau wa kujadili Mpango Kazi wa Kuendesha Shughuli za Serikali kwa Uwazi (OGP)  wa Awamu ya Tatu,  uliofanyika katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es Salaam. 


Katibu Mkuu Ikulu Bw. Peter Ilomo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa kujadili Mpango Kazi wa Kuendesha Shughuli za Serikali kwa Uwazi ( OGP)  wa Awamu ya Tatu  uliofanyika katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es salaam.  Bw. Ilomo alifungua mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb).


Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan P. Mlawi (katikati) akifafanua hoja kuhusu Mpango Kazi wa Kuendesha Shughuli za Serikali kwa Uwazi ( OGP)  wa Awamu ya Tatu wakati wa mkutano wa wadau wa kujadili mpango huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es Salaam. 


Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan P. Mlawi akisisitiza jambo kuhusu Mpango Kazi  wa Kuendesha Shughuli za Serikali kwa Uwazi ( OGP)  wa Awamu ya Tatu wakati wa mkutano wa wadau wa kujadili mpango huo, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es Salaam.