Walimu 450 walioajiriwa Shule Binafsi waomba Kurudi Serikalini | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

9/7/16

Walimu 450 walioajiriwa Shule Binafsi waomba Kurudi SerikaliniWalimu 450 waliokuwa wameajiriwa na Serikali na kuzikimbia ajira zao na kwenda kufundisha katika shule binafsi wameiandikia Serikali barua za kuomba kurejea katika ajira zao.
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Suleiman Jafo amesema maombi hayo yamekuja katika kipindi hiki ambacho serikali inaendelea kufanya maboresho ya maslahi na kiutendaji kwenye muundo wa utumishi wa umma.
Ni sehemu ya walimu waliohitimu mafunzo ya umahiri katika ufundishaji wa stadi za kujua kusoma kuandika na kuhesabu kwa wanafunzi wa darasa la tatu na nne mafunzo yaliyohusisha walimu 22,995 katika vituo 16 nchini ambapo katika kituo cha mikoa ya Mbeya na Songwe walimu 2,205 wameshiriki.
Akifunga mafunzo hayo katika chuo cha Ualimu Tukuyu wilayani Rungwe kwa niaba vituo vyote vya mafunzo nchini, Mheshimiwa Jafo amewataka watumishi wa Umma wakiwemo walimu kulinda ajira zao kwa kuwa maboresho yanayo endelea kufanywa na serikali yatasababisha watu wengi kutaka ajira za umma na hawatazipata.
Mafunzo hayo ambayo yamehusisha uchambuzi wa Mtaala mpya wa Elimu wa mwaka 2016, uchambuzi wa miongozo ya kufundishia, maandalizi ya somo na umahiri wa utambuzi wa somo kwa wanafunzi, yameratibiwa na Wakala wa Maendeleo ya Uongozi waa Elimu nchini, ADEM
Kwa mujibu wa Afisa Emuli Taaluma wa mkoa wa Mbeya , Gerald Kifyas pamoja na walimu waliohitimu mafunzo hayo kwa mikoa ya Mbeya na Songwe wamesema stadi walizo zipata zitasaidia kuboresha taaluma.
#StarTvTanzania

google+

linkedin