9/4/16

Walimu Watakaokataa Kwenda Kufundisha Maeneo ya Vijijiji Kuchukuliwa Hatua Kali.

Image result for Therecia Mahongo
Baada ya kukithiri kwa tabia ya walimu kukataa kufundisha kwenye shule zilizopo maeneo ya pembezoni katika wilaya ya Karatu mkuu wa wilaya hiyo Therecia Mahongo ameagiza kusimamishwa kazi na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa watumishi watakaokataa kwenda katika maeneo ya vijijiji kwakuwa wamechangia kushuka kwa kiwango cha elimu.
Mkuu wa wilaya ya Karatu Therecia Mahongo ametoa kauli hiyo wakati wadau wa elimu kutoka sekta binafsi na taasisi za dini walipokabidhi vyumba vya madarasa vyoo na zaidi ya madawati mia sita katika shule za tarafa za Eyasi na Mang’ola ambako kuna upungufu mkubwa wa vifaa katika shule za msingi na sekondari na mkuu huyo kudai kuwa haiwezekana taasisi binafsi zitoe mchango mkubwa na watumishi wawe kikwazo kwa maendeleo ya watoto watanzania.

Baadhi ya walimu wa shule zilizopatiwa msaada wamesema utasaidia kupunguza changamoto ya wanafunzi kurundikana kwenye darasa na madawati na kwamba kitendo cha walimu kukataa kuripoti kwenye shule hizo kunaathiri wanafunzi kwakuwa kuna baadhi ya shule zina wanafunzi wengi lakini walimu hawazidi wawili.

Kwa upande wao wadau wa elimu waliyotoa msaada huo wamesema wamekuwa wakitoa msaada wa vyumba vya madarasa madawati na vitendeakazi lakini wanavunjwa moyo wanaposikia walimu wanakataa kwenda kufundisha kwenye shule hizo.
 
chanzo: ITV
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts