Wanafunzi zaidi ya 600 waiomba serikali kuharakisha ujenzi wa mabweni mkoani Tanga. | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

9/4/16

Wanafunzi zaidi ya 600 waiomba serikali kuharakisha ujenzi wa mabweni mkoani Tanga.

Wanafunzi zaidi ya 600 waliopo wilaya za Mkinga na Muheza wameiomba serikali kuharakisha zoezi la kuwajengea mabweni katika shule zao kufuatia baadhi yao kupewa ujauzito huku wengine kulazimika kuacha shule kwa sababu ya utoro kufuatia kata zao kutokuwa na shule za sekondari.
Wakizungumza na Waandishi wetu wilayani Mkinga baadhi ya wananfunzi wa shule ya sekondari Maramba wamemshukuru Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kwa kuondoa kero ya michango na ada shuleni lakini ukosefu wa mabweni ni changamoto kubwa inayosababisha baadhi ya wanafunzi kusitishwa masomo yao .

Kwa upande wao wanafunzi wa shule ya sekondari Nkumba iliyopo kata ya Nkumba wilayani Muheza wamesema wanalazimika kutembea umbali wa kilomita 24 kutoka vijiji vya Kiwanda, Mangubu na Tongwe hadi tarafa ya Nkumba kwa sababu kata mbili za Tongwe na Bombani kutegemea shule moja iliyopo tarafa ya Nkumba.

Kufuatia hatua hiyo walimu wa shule hizo wameiomba serikali kuangalia kwa jicho la huruma tatizo hilo kwa sababu wanafunzi wanajitahidi kuongeza jitihada huku walimu wakiwadhibiti kuepuka kuingia kwenye vishiwishi lakini bado hali ni tete hadi watakapohifadhiwa katika mabweni. 
 chanzo: ITV

google+

linkedin