9/9/16

Watatu Wapoteza Fahamu Baada ya Moto Kuunguza Nyumba Walimokuwa Wamehifadhi Vibubu Vyao Kwaajili ya Vikoba


Watu watatu wamepoteza fahamu baada ya Nyumba waliyokuwa wakikutana kwa Ajili ya mchezo wa Kuweka na kukopa Kuteketea Moto na kukuta kisanduku cha Kuhifadhia Fedha zao za Kicoba kuungua moto.

Moto huo Ulionza majira ya saa 9 jioni Uliotokana na Kilichoelezwa kuwa ni Hitilafu ya Umeme kutokana na kuzimika zimika mara kwa mara Katika Maeneo mbalimbali ya Mji wa Lindi hii Leo Hali iliyosababisha akina mama 3 kupoteza Fahamu na Kukimbizwa katika Hospital ya Rufaa ya Sokoine, Manispaa ya Lindi


Wakiongea na Channel Ten Baadhi ya Mashuhuda wa Tukio Hilo akiwemo Mmiliki wa Nyumba Hiyo Iliyopo Msonabarini Kata ya Msinjahili ,Hussein Chosso walieleza walivyobaini Moto mara Ulipoanza kabla ya Moto Huo Kudhibitiwa na Kikosi cha zimamoto cha mjini Lindi


Msaidizi Kikosi cha Zimamoto
Kwa hivi karibuni Ili ni tukio la Pili La Moto Unaosemekana Kusababishwa na Hitilafu za Umeme na Kusababisha Shule ya Sekondari nayo Kuunguamajengo na Thamani Kadhaa

Abdulazizi Ahmed -Lindi
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts