9/2/16

Watendaji Washushwa Vyeo Kwenye Sakata la Wanafunzi HewaWilaya ya Longido mkoani Arusha, imebaini wanafunzi hewa 4,081 ambao kati ya Januari na Julai, wametumiwa Serikali Sh195.4 milioni.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Daniel Chongolo (pichani) akizungumza na waandishi wa habari jana, aliagiza kuvuliwa nyadhifa walimu wakuu wa shule 25 za msingi, sekondari mbili na waratibu elimu kata 11.

“Nimeagiza ufanyike uchunguzi wa kina na wote ambao wamehusika kula Sh195 milioni wachukuliwe hatua kali za kisheria,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Longido, Jumaa Mhina alisema wamewaandikia barua za kuwashusha vyeo wakuu wote wa shule ambazo zimebainika kuwa na wanafunzi hewa.

chanzo: Mwananchi
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm