9/7/16

Watumishi saba waliosimamishwa Iramba warejeshwa

Jumla ya watumishi saba wa halmashauri ya Iramba mkoani Singida waliosimamishwa kazi Februari 26 mwaka huu, wamerejeshwa kazini baada ya Serikali kujiridhisha kuwa hawana hatia dhidi ya tuhuma walizokuwa wakituhumiwa.

Waliorejeshwa kwenye nafasi zao kwenye hospitali ya wilaya ya Iramba ni mganga msaidizi mwandamizi wa meno, Dk Timoth Sumbe, makatibu wa afya Kaleb Ngughu, Sundy Alphonce, Grace Nganga, mratibu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambaye pia ni ofisa maendeleo ya jamii mwandamizi, Silvery Maganza.

Watumishi hawa walikuwa wakituhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka, ambapo walitumia zaidi ya Sh 145 milioni za NHIF),kinyume na taratibu.

NHIF ilitoa fedha hizo Julai Mosi 2013 kipindi wilaya ya Iramba ilijumuisha na jimbo la Iramba mashariki kwa wakati huo, ambapo lilipanndishwa hadhi na kuwa wilaya ya Mkalama.


Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhaluha alisema kwa kutumia vyombo vya usalama ikiwemo Takukuru na jeshi la polisi, vilifanya uchunguzi wa kina na kubaini kuwa watuhumiwa wote saba hawana hatia.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts