9/26/16

Waziri Kairuki atoa ofa kwa wanafunzi




Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki ametoa zawadi ya ada kwa masomo ya kidato cha tano na sita kwa wanafunzi watakaofanya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha nne mwaka huu.


Zawadi hiyo ameitoa leo katika mahafali ya 14 ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Barbro Johansson Model Girls, iliyopo Luguruni jijini Dar es Salaam.


Kairuki amesema zawadi hiyo ameitoa kupitia mfuko wake wa Angela Kariuki Scholaship Fund.


"Nitasomesha wanafunzi wawili ambao watafanya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha nne, na kuamua kurudi kwa mara nyingine kusoma masomo ya kidato cha tano na sita hapa Barbro Johansson Model Girls," alisema Kairuki.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts